Nasihi Tuache Ukatili Dhidi ya Binadamu Wenzetu

Story by Joy Achieng, St. Hannah High School

Ulanguzi wa binadamu ni nini? Hii ni nyendo au wendaji wa watu au kuwateka nyara bila idhini yao au kama hawafahamu. Hii si mara ya kwanza tunaskia kuhusu haya. Wengi wetu tumeyasikia haya lakini kupuuzilia na kuyatupa mambo haya katika kaburi la sahau. Mambo haya yanatendeka haswa katika bara la Afrika. Njia nazo ni nyingi kama huko pwani, njia ni mzomzo. Watu hawa wanatolewa shimoni huko Mombasa, Kenya, wakipelekwa Pemba na Pangani nchini Tanzania halafu Msumbiji kasha Afrika kusini. Jambo la kushtusha ni kuwa , wanawake wengine wanawauza wasichana kutoka Tanzania mpaka Lubumbashi ama Kisangani humo Demokrasia ya Kongo na wazungu kuwanunua.

Sababu zinazochangia ulanguzi wa binadamu katika bara la Afrika ni, kwanza, umaskini na ukosefu wa kazi. Umaskini na ukosefu wa kazi unawatia motisha waja hawa ili angalau wapate cha kuwalisha  wanao. Wanawake na wasichana wanafanywa kuwa na hadhi ndogo katika jamii. Hii inaongeza chanzo cha wanawake na wasichana kudhulumiwa. Vita barani Afrika navyo , vinachangia sana wana wenye umri mdogo kurutika katika mashirika ya askari wahalifu, ambao kazi yao ni kuua. Sababu nyingine nazo ni masomo kukosekana, ufisadi na ukahaba katika utalii.

Kwa nini binadamu mwenye akili timamu amfanyie hivi binadamu mwenzake au mwana mwenye umri sawia na mwanawe? Sababu ni wazi kama pengo. Fedha , pesa mabunda ya noti. Hii ndiyo sababu kuu ya utendaji huu.  Binadamu ametambulika kutaka kuwa lodi mwenye mali kama njugu. Binadamu wengi walipewa vyuma badala ya mioyo kwa sababu hawana huruma hata

Ningependekeza suluhisho mbalimbali ili maarifa kuhusu ulanguzi wa binadamu uenee katika pembe zote za dunia. Ningependa, shirika kadha wa kadha lijitokeze ili liwapiganie watu wanaokumbwa na balaa hii. Wasichana kwa wanawake. Wavulana kwa wazee. Wote watendewe haki na usawa wa jinsia uzingatiwe. Wengi wetu tuwatembelee wahusika walio dhulumiwa na tuwaletee habari hii umma. Kwa kufanya hivi, itawafanya wengi wajue na wawe waangalifu na kuripoti wakiona mambo si mrama. Katika boda za nchi, usalama uimarishwe na uwe wa hali ya juu. Polisi wafisadi waondolewe kwenye eneo hilo na polisi wa wananchi wapewe cheo hicho. Vilevile, viongozi wa nchi ambayo wanajishugulisha na uhalifu huu, waondolewe katika vyeo vyao. Suluhisho la mwisho ni kuwaelimisha watu hawa.

Mashirika yaliyojishugulisha, naomba yajikaze kisabuni ili watu hawa wasiendelee kuteseka nchini kwao. Viongozi wa nchi hizi pia ningewaomba wajaribu kukomesha visa hivi, ili viache kuwa tatizo barani Afrika. Viongozi tena waziweke sheria ambayo inasaidia mashirika kutekeleza jukumu lao. Tukiwa na serikali ambayo inatia motisha mashirika hayo, basi tujue tunasonga mbele kama jeshi la wokovu.

Mbali na mashirika na serikali, ningependa sana watu, wahanga na waja ambao hawajakumbwa na haya, wote tuungane pamoja ili tuukomeshe ulanguzi wa watu. Tuuzidishe usawa wa jinsia na tupendane kama ndugu wenye damu moja au kuzaliwa na mama moja. Umoja ni nguvu na utengano ni udhalifu. Huu uwe wito wetu daima. Mola mwenye Baraka zisizo na kifani, atatubariki na kutunyeshea mvua za Baraka siku zote.

 

This story is part of the campaign by Fern Poetry to spread counter trafficking awareness through poetry. Once the poem campaign in finished, students create their own poems or stories depending on how they received the CTIP message.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: